Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 10

At-Tahrim 66:10

التحريم

ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱمْرَأَتَ نُوحٍ وَٱمْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَـٰلِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا وَقِيلَ ٱدْخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّٰخِلِينَ

Maana

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale waliokufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawafanyia uhaini waume zao, nao wasiwafae kitu kutokana na Mwenyezi Mungu. Na ikasemwa: 'Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia! [10]

[10] Mwenyezi Mungu ametaja hali ya ajabu inayo juulikana kuwa ni hali zinazo fanana kwa wanao kufuru. Nayo ni hali ya mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Hao walikuwa chini ya ulinzi wa waja wawili katika waja wema. Nao wakawakhuni kwa kupanga njama dhidi yao, na kufichua siri zao kwenda wambia kaumu zao. Na waja wema wawili hawakuweza kuwakinga wake zao kwa lolote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wakaambiwa hao wake wawili walipo angamizwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anapiga mfano wa hali ya makafiri katika kutangamana kwao na Waislamu, na kuwa karibu nao na kwamba hilo halitawanufaisha kitu, kwa kuwa wamemkufuru Allah Mtukufu, kuwa ni kama hali ya mke wa Nabii wa Allah Mtukufu, Nûḥ, na mke wa Nabii wa Allah Mtukufu, Lûṭ, kwa kuwa wote wawili walikuwa chini ya hifadhi ya ndoa ya waja wawili wema miongoni mwa waja wetu, wakawafanyia hao waume zao uhaini wa kidini, kwani wote wawili walikuwa makafiri! Mitume wawili hawa hawakuweza kuwatetea wake zao na adhabu ya Allah Mtukufu, na wakaambiwa wake wawili hao, «Ingieni Motoni pamoja na wenye kuingia huko.» Katika kupiga mfano huu pana dalili ya kwamba kuwa karibu na Manabii na watu wema hakufai kitu iwapo mtu mwenyewe ana matendo mabaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net