At-Tahrim 66:11
التحريموَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱمْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ٱبْنِ لِى عِندَكَ بَيْتًا فِى ٱلْجَنَّةِ وَنَجِّنِى مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِۦ وَنَجِّنِى مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale walioamini - mkewe Firauni, aliposema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba katika Bustani ya mbinguni, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu. [11]
[11] Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano kwa Waumini kisa cha mke wa Firauni alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba karibu na rehema yako Peponi, na uniokoe na utawala wa Firauni na vitendo vyake vilivyo pita mipaka katika dhulma, na uniokoe na kaumu ya wanao fanya uadui!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Anapiga mfano wa hali ya Waumini- waliomuamini Allah Mtukufu, wakamuabudu Peke Yake na wakazifuata Sheria Zake kivitendo na kwamba hakuwadhuru kule kutangamana kwao na makafiri katika maingiliano yao- kuwa ni kama hali ya mke wa Fir‛awn aliyekuwa kwenye hifadhi ya ndoa ya aliyekuwa muovu mno miongoni mwa wale waliomkufuru Allah Mtukufu, na hali yeye alikuwa anamuamini Allah Mtukufu, pindi aliposema, «Mola wangu! Nijengee Nyumba huko kwako Peponi, na uniokoe na utawala wa Fir‛awn na ukafiri wake na yale matendo maovu yanayotokana na yeye, na uniokoe na watu wenye kumfuata katika udhalimu na upotevu, na uniokoe na mateso yao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net