Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 12

At-Tahrim 66:12

التحريم

وَمَرْيَمَ ٱبْنَتَ عِمْرَٰنَ ٱلَّتِىٓ أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَـٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتْ مِنَ ٱلْقَـٰنِتِينَ

Maana

Na Mariamu binti wa Imrani, aliyelinda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu. [12]

[12] Na Mwenyezi Mungu amewapigia Waumini mfano wa Mariamu binti wa Imrani, ambaye amehifadhi utupu wake, tukampulizia humo katika roho yetu, akashika mimba ya Isa. Naye akayasadiki maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni amri zake, na makatazo yake, na Vitabu vilivyo teremshwa juu ya Mitume wake. Na yeye alikuwa miongoni mwa idadi walio dumu juu ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. (Huku kupuliziwa Mariamu roho ya Mwenyezi Mungu si kiroja, kwani wanaadamu wote wamepuliziwa kadhaalika. Soma Surat Al-H'ijr Aya 28-29 inapo simuliwa alipo umbwa mtu na akapuliziwa kutokana na roho ya Mwenyezi Mungu.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Anapiga mfano kwa walioamini. Mfano wenyewe ni Maryam binti ‛Imrān aliyeihifadhi tupu yake na akailinda na uzinifu, basi Allah Mtukufu Akamuamrisha Jibrili, (amani imshukie), apulize kwenye mfuko wa nguo yake. Na ule mpulizo ukafika kwenye kizazi chake. Hapo akabeba mimba ya ‘Ῐsā, (amani imshukie), akayaamini maneno ya Mola wake, akafuata kivitendo Sheria Zake Alizozipasisha kwa waja Wake, na vitabu Vyake Alivyoviteremsha kwa Mitume Wake, na akawa ni miongoni mwa wenye kumtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net