Al-Mulk 67:1
الملكتَبَـٰرَكَ ٱلَّذِى بِيَدِهِ ٱلْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [1]
[1] Ametukuka, na amezidi baraka zake Mwenye kumiliki peke yake uwezo wa kuendesha mambo ya viumbe vyote. Na Yeye, juu ya kila kitu, anao uwezo ulio timia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zimekithiri kheri za Allah Mtukufu na wema Wake kwa viumbe Vyake, Ambaye mkononi Mwake upo ufalme wa duniani na Akhera na mamlaka ya viwili hivyo, Anapitisha amri Yake na uamuzi Wake kwenye mamlaka Yake hayo, na Yeye kwa kila jambo ni Muweza. Faida inayopatikana katika aya hii ni kuwa inathibitisha sifa ya mkono kwa Allah Mtukufu Aliyetakasika na kutukuka, kwa namna inavyonasibiana na utukufu Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net