Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 8

At-Tahrim 66:8

التحريم

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ تُوبُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ يَوْمَ لَا يُخْزِى ٱللَّهُ ٱلنَّبِىَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَـٰنِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَٱغْفِرْ لَنَآ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Bustani zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: 'Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [8]

[8] Enyi mlio amini! Rejeeni kwa Mwenyezi Mungu, muache madhambi yenu, mrejee kweli kweli kwa ikhlasi. Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu, na akakutieni Peponi kwenye kupita mito chini ya majumba yake na miti yake, Siku atakayo inyanyua Mwenyezi Mungu hadhi ya Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao hao itakuwa inakwenda mbele yao, nayo itakuwa kuliani mwao, nao watakuwa wakisema kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu: Ewe Bwana wetu, Mwenye kumiliki mambo yetu! Tutimizie nuru yetu, mpaka tuongoke kufikia Peponi. Na tusamehe dhambi zetu. Hakika Wewe ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Acheni madhambi yenu na mrudi kwenye kumtii Allah Mtukufu, kurudi kwa mwisho kusikokuwa na ufanyaji maasia tena kwa, kutarajia Mola wenu Awafutie maovu ya matendo yenu, na Awaingize kwenye mabustani ya Peponi ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito ya maji, Siku ambayo Allah Mtukufu Hatamfedhehi Nabii na walioamini pamoja naye wala hatawatesa, bali Atavipandisha juu vyeo vyao. Nuru ya watu hawa itakuwa inatembea mbele yao na kuliani mwao huku wakisema, «Mola wetu! Tukamilishie nuru yetu mpaka tuvuke Sirāṭ na tuongoke njia ya kwenda Peponi, na utusamehe na uyatupilie mbali madhambi yetu na uyasitiri, kwani wewe Kwa hakika ni Muweza kila kitu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net