Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 7

At-Tahrim 66:7

التحريم

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَا تَعْتَذِرُوا۟ ٱلْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda. [7]

[7] Wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama: Msitafute udhuru leo! Hapana shaka mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wataambiwa wale waliokanusha kwamba Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki na wakamkufuru, watakapoingizwa Motoni, «Msitafute nyudhuru Siku ya Leo, ukweli ni kwamba nyinyi mnapewa malipo ya yale ambayo mlikuwa mkiyafanya duniani».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net