At-Tahrim 66:6
التحريميَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَـٰٓئِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ
Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu kutokana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa. [6]
[6] Enyi mlio amini! Jihifadhini nafsi zenu na ahali zenu na Moto, ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanao simamia kazi yake na kuwaadhibu waliomo humo ni Malaika wakali, na wana nguvu katika muamala wao. Na wao hutekeleza lile wanalo amrishwa, wala hawakawilishi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Zilindeni nafsi zenu kwa kuyatenda yale ambayo Amewaamrisha kwayo Allah Mtukufu na kuyaepuka yale ambayo Amewakataza nayo, na walindeni watu wenu kwa kile mnachotumia kujilinda nyinyi wenyewe na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Watasimamia kuadhibiwa watu wa Motoni Malaika wenye nguvu walio thabiti katika usimamizi wao, wasioenda kinyume na Allah Mtukufu katika maamrisho Yake, na wanaotekeleza yale wanayoamrishwa nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net