Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 5

At-Tahrim 66:5

التحريم

عَسَىٰ رَبُّهُۥٓ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُۥٓ أَزْوَٰجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَـٰتٍ مُّؤْمِنَـٰتٍ قَـٰنِتَـٰتٍ تَـٰٓئِبَـٰتٍ عَـٰبِدَٰتٍ سَـٰٓئِحَـٰتٍ ثَيِّبَـٰتٍ وَأَبْكَارًا

Maana

Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanyenyekevu, Waumini, watawa, waliotubu, wenye kushika ibada, wafanyao heri, waliowahi kuoleka na wale ambao hawajawahi kuoleka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanynyekevu, Waumini, wat'awa, walio tubu, wenye kushika ibada, wafanyao kheri, wajane na wanawari. [5]

[5] Asaa Mola wake Mlezi akikuacheni, enyi wakeze, atamwoza badala yenu wake wengine walio wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu, wenye kusadiki kwa nyoyo zao, wanyonge mbele ya Mwenyezi Mungu, wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa toba, wenye kumuabudu kwa kujidhalilisha kwake, wendao kila njia za ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, wajane na bikra.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Linalotarajiwa kwa Mola wake iwapo atawaacha nyinyi, (enyi wake zake), ni amuoze, badala yenu, wake wanyenyekevu kwa Allah Mtukufu, wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wenye kumtii Allah Mtukufu, wenye kurudi kwenye yale anayoyapenda Allah Mtukufu ya kumtii, wenye kumuabudu kwa wingi, wenye kufunga sana, wakiwa wake wakuu miongoni mwao na wanawali.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net