At-Tahrim 66:4
التحريمإِن تَتُوبَآ إِلَى ٱللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَـٰهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ مَوْلَىٰهُ وَجِبْرِيلُ وَصَـٰلِحُ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۖ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ
Kama nyinyi wawili hamtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia. [4]
[4] Mkirejea nyinyi wawili kwa Mwenyezi Mungu nanyi mmejuta basi itakuwa mmefanya waajibu wenu wa kutubu, kwa sababu nyoyo zenu zilikuwa zimeacha jambo analo lipenda Mtume wa Mwenyezi Mungu, nalo ni kuweka siri. Na ikiwa mtasaidiana kinyume chake kwa mambo ya kumuudhi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msaidizi wake, na Jibrili, na Waumini wanao sifika kwa wema, na Malaika baada ya msaada wa Mwenyezi Mungu nao ni wenye kumsaidia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Iwapo mtarudi kwa Allah Mtukufu (ewe Ḥafṣah na ‛Ᾱishah) basi yatakuwa yamepatikana kwenu yanayopelekea kukubaliwa toba yenu, kwa kuwa nyoyo zenu zilielekea kwenye kuyapenda yale aliyoyachukia Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ya kutoa siri yake. Na mtakaposaidiana kuwa dhidi yake kwa kufanya yanayomuudhi, basi Allah Mtukufu Ndiye Msimamizi wake na Mtetezi wake na Jibrili na Waumini wema. Na Malaika, baada ya usaidizi wa Allah Mtukufu, ni wasaidizi wake na watetezi wake dhidi ya yoyote anayemuudhi na kumfanyia uadui.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net