Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 66 · Aya ya 3

At-Tahrim 66:3

التحريم

وَإِذْ أَسَرَّ ٱلنَّبِىُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَٰجِهِۦ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِۦ وَأَظْهَرَهُ ٱللَّهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُۥ وَأَعْرَضَ عَنۢ بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِۦ قَالَتْ مَنْ أَنۢبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِىَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْخَبِيرُ

Maana

Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipolitangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyingine. Alipomwambia hayo, huyo mke akasema: 'Ni nani aliyekwambia haya?' Mtume akasema: 'Kaniambia Yule ajuaye zaidi, Mwenye habari zote!'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Nabii alipo mwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipo litangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipo mwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliye kwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye khabari zote! [3]

[3] Na taja pale Nabii alipo msimulia jambo kwa siri mmoja katika wake zake, na alipo ifichua. Na Mwenyezi Mungu akamjuvya Nabii wake kuwa imefichuliwa. Akamjuvya baadhi, na akamzuilia - kwa staha - baadhi nyengine. Alipo mjuvya, akasema yule mke: Nani aliye kwambia haya? Akasema Nabii: Ameniambia Mwenye kujua kila kitu, asiye fichika kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi Mtume alipompa siri mke wake Hafṣah, (radhi za Allah Mtukufu zimshukie), ya mazungumzo fulani, na yeye alipomwambia maneno hayo mke mwenzake ‛Ᾱishah, radhi za Allah Mtukufu zimshukie, na Allah Mtukufu Akamjulisha Mtume Wake kuwa mkewe ameitoa siri yake, alimjulisha Hafṣah sehemu ya maneno aliyoyatoa na akayanyamazia mengine asimwambie kwa kuchunga heshima. Basi Mtume alipomwambia Hafṣah yale mazungumzo aliyoyatangaza, alisema hafsah, «Ni nani aliyekwambia maneno hayo?» Akasema Mtume, «Aliyeniambia hayo ni Allah Mtukufu, Aliye Mwingi wa ujuzi na utambuzi, Ambaye hakifichiki Kwake chenye kujificha chochote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tahrim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net