At-Tahrim 66:2
التحريمقَدْ فَرَضَ ٱللَّهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَـٰنِكُمْ ۚ وَٱللَّهُ مَوْلَىٰكُمْ ۖ وَهُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ
Hakika Mwenyezi Mungu amekupeni Sheria ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sharia ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [2]
[2] Amekuwekeeni Sharia ya kuondoa viapo vyenu kwa kafara. Na Mwenyezi Mungu ni Bwana wenu, Mwenye kutawala mambo yenu, na Yeye ni Mtimilivu wa ujuzi, basi anakuwekeeni Sharia zenye kheri yenu, naye ni Mwenye hikima katika kuweka Sharia zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Amepasisha Allah Mtukufu kwenu, (enyi Waumini), kuvihalalisha viapo vyenu kwa kuvitolea kafara. Kafara yenyewe ni kuwalisha masikini kumi au kuwavisha au kuacha mtumwa huru. Na asiyepata cha kutoa, basi afunge siku tatu. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuwanusuru nyinyi na kuyasimamia mambo yenu. Na Yeye Ndiye Mjuzi wa mambo yanayowafaa Akayapitisha kwenu, Ndiye Mwingi wa hekima kwenye maneno Yake na matendo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net