Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 3

At-Talaaq 65:3

الطلاق

وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَـٰلِغُ أَمْرِهِۦ ۚ قَدْ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَىْءٍ قَدْرًا

Maana

Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu, Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake. [3]

[3] Na atamtengezea sababu za kupata riziki kwa jiha ambazo hata hazimpitikii katika fikra zake. Na mwenye kumwachia mambo yake yote Mwenyezi Mungu basi Yeye ni Mwenye kumtosha, hana haja ya mwengine. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimiza alitakalo, ni Mwenye kutekeleza alipendalo. Amejaalia kila kitu na wakati wake, wala haupitikii, na kipimo hakivuki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na atamuwepesishia njia za kupata riziki kwa namna ambayo haikupita akilini mwake wala haikuwa kwenye hesabu zake. Na yoyote atakayemtegemea Allah Mtukufu basi Yeye Atamtosheleza kwa kumuondoshea yale yanayomkera katika mambo yake yote. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kulifikia jambo Lake, Hapitwi na kitu chochote wala haelemewi na kitu chochote akitakacho, hakika Allah Mtukufu Amekiwekea kila kitu muda wake wa kuisha na kipimo ambacho kitu hicho hakiwezi kukipita.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net