Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 65 · Aya ya 2

At-Talaaq 65:2

الطلاق

فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا۟ ذَوَىْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا۟ ٱلشَّهَـٰدَةَ لِلَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مَخْرَجًا

Maana

Basi wanapofikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hayo anaaidhiwa kwayo anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, humtengezea njia ya kutokea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. [2]

[2] Wakikaribia walio achwa mwisho wa eda zao warejeeni mkae nao kwa wema na ihsani, au farikianeni nao bila ya madhara. Na washuhudisheni kuwarejea na kufarikiana watu wawili waadilifu miongoni mwenu, na toeni ushahidi kwa mujibu wake kwa kumsafia Mwenyezi Mungu. Hayo mliyo amrishwa ndiyo anayo waidhiwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kumkhofu Mwenyezi Mungu akazishika amri zake na akaepuka makatazo yake atamjaalia njia ya kutokana na kila dhiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi kipindi cha eda ya wanawake waliopewa talaka kinapokaribia kumalizika, basi warudieni na muishi nao kwa wema pamoja na kuwapatia matumizi, au waacheni pamoja na kuwatekelezea haki zao bila kuwafanyia mambo ya kuwadhuru. Na wekeni mashahidi mnaporejeana na mnapoachana, wanaume wawili waadilifu miongoni mwenu. Na toeni, (enyi mashahidi), ushahidi wenu kwa ajili ya Allah Mtukufu tu na sio kwa kitu kingine. Hilo ambalo Allah Mtukufu Amewaamrisha kwalo anawaidhiwa nalo yule anayemuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho. Na yoyote atakayemuogopa Allah Mtukufu akayafuata kivitendo yale ambayo Amemuamrisha nayo na akayaepuka yale ambayo Amemkataza nayo, atamuwekea njia ya kutoka kwenye kila dhiki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Talaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net