At-Talaaq 65:4
الطلاقوَٱلَّـٰٓـِٔى يَئِسْنَ مِنَ ٱلْمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمْ إِنِ ٱرْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَـٰثَةُ أَشْهُرٍ وَٱلَّـٰٓـِٔى لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُو۟لَـٰتُ ٱلْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مِنْ أَمْرِهِۦ يُسْرًا
Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba, eda yao ni mpaka watakapozaa. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi. [4]
[4] Na wenye eda ya talaka miongoni mwa wanawake walio sita kuingia myezini kwa utu uzima, kama hawajui wahisabu vipi eda yao, basi eda yao ni miezi mitatu. Na wale ambao hawaingii hedhi kabisa ni kadhaalika. Na wenye mimba, eda yao inakwisha wanapo jifungua. Na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, na akazitimiza hukumu zake Mwenyezi Mungu atamsahilishia mambo yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanawake walioachwa ambao damu zao za hedhi zimekatika kwa utu uzima wao, mkitatizika mkawa hamjui: ni nini hukumu yao? Basi, eda yao ni miezi mitatu. Na wanawake wadogo ambao hawajaingia damuni, eda yao ni miezi mitatu vilevile. Na wanawake wajawazito, eda yao inamalizika pale wanapozaa. Na yoyote atakayemuogopa Allah Mtukufu na akatekeleza hukumu Zake, Atamfanyia mambo Yake yawe mepesi duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net