At-Taghaabun 64:9
التغابنيَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ ٱلْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلتَّغَابُنِ ۗ وَمَن يُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعْمَلْ صَـٰلِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُدْخِلْهُ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
Siku atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko. Hiyo ni siku ya kupunjana. Na anayemuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yenye kupitiwa kati yake mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku atakayo kukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko; hiyo ni siku ya kupunjana. Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Mabustani yenye kupitiwa kati yake na mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [9]
[9] Siku atapo kukusanyeni katika Siku ya Mkusanyo wa walio tangulia mwanzo na walio kuja mwisho, akulipeni kwa vitendo vyenu! Siku hiyo ndiyo Siku ya Taghaabun, Kupunjana, kutapo dhihiri kupunjika kwa makafiri kwa kuacha Imani, na kupunjika Waumini kwa kupuuza kuongeza ut'iifu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema atamwondolea maovu yake, na atamtia katika Bustani zenye kupita kati yake mito, wakae humo milele. Malipo hayo ndio kufuzu kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ikumbukeni Siku ya Mkusanyo ambayo Allah Mtukufu Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho. Siku hiyo ambayo ina mpunjano na mtengano kati ya viumbe: Waumini wawapunje makafiri na wenye kuasi, na wao hao (makafiri na waasi) iwadhihirikie wazi kuwa wao ndio waliopata hasara. Basi wenye Imani wataingia Peponi kwa rehema za Allah Mtukufu, na wenye ukafiri wataingia Motoni kwa uadilifu Wake. Na mwenye kumuamini Allah Mtukufu na akafanya matendo ya utiifu Kwake, Atamfutia dhambi zake na Amtie kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito ya maji, hali ya kukaa milele humo. Kukaa milele huko Peponi ndiko kufaulu kukubwa ambako hakuna kufaulu kushinda huko.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net