Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 8

At-Taghaabun 64:8

التغابن

فَـَٔامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلْنَا ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Maana

Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyoiteremsha. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyo iteremsha. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [8]

[8] Basi msadikini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ongokeni kwa kuifuata Nuru tuliyo mteremshia hata akakufahamisheni kwa uwazi kuwa kufufuliwa kunakuja bila ya shaka yoyote. Na Mwenyezi Mungu ana ujuzi wa kutumia kwa yote yanayo tokana nanyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi muaminini Allah Mtukufu na Mtume Wake, (enyi washirikina), na mjiongoze kwa Qur’ani Aliyomteremshia Mtume Wake. Na Allah Mtukufu kwa mnayoyafanya ni Mtambuzi, hakuna kinachofichika kwake cha matendo yenu na maneno yenu, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwa hayo Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net