Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 7

At-Taghaabun 64:7

التغابن

زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَن لَّن يُبْعَثُوا۟ ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّى لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ

Maana

Wale waliokufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyoyatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu. [7]

[7] Makafiri wamedai kwa uwongo kwamba hawatafufuliwa baada ya kufa kwao. Ewe Muhammad! Waambie: Mambo sio kama mnavyo dai nyinyi. Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka yoyote nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa kwenu, na hapana shaka yoyote kuwa mtaambiwa mliyo yatenda duniani. Kisha mtalipwa kwayo. Na huko kufufuliwa, na kuhisabiwa, na kulipwa, ni jambo sahali na jepesi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walidai wale waliomkanusha Allah Mtukufu kwamba wao hawatatolewa kwenye makaburi yao baada ya kufa. Waambie, (ewe Mtume), «Ndio. Naapa kwa Mola wangu! Mtatolewa makaburini mwenu mkiwa hai, kisha mtapewa habari ya yale mliyoyafanya duniani. Na hilo kwa Allah Mtukufu ni sahali na rahisi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net