At-Taghaabun 64:6
التغابنذَٰلِكَ بِأَنَّهُۥ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَقَالُوٓا۟ أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا۟ وَتَوَلَّوا۟ ۚ وَّٱسْتَغْنَى ٱللَّهُ ۚ وَٱللَّهُ غَنِىٌّ حَمِيدٌ
Hayo ni kwa kuwa Mitume wao walikuwa wakiwajia kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: ʻHivyo binadamu ndio atuongoze?ʼ Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, Msifiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo binaadamu ndio atuongoe? Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, naye ni Msifiwa. [6]
[6] Masaibu hayo yaliyo wapata ni kwa sababu Mitume wao waliwajia na miujiza iliyo dhaahiri, nao wakasema kwa kukanya: Ati atujie mtu kama sisi kutuongoza? Wakakanya kuwa watafufuliwa. Wakaiacha Haki. Mwenyezi Mungu akadhihirisha kuwa hana haja na imani yao kwa kuwaangamiza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ukwasi wake (kujitosha kwake), si Mwenye kuwa na haja na viumbe vyake. Ni Mwenye kustahiki kusifiwa na kuhimidiwa kwa uzuri wa neema zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hayo yaliyowapata duniani na yatakayowapata kesho Akhera ni kwamba wao walikuwa wakijiliwa na Mitume wa Allah Mtukufu na alama za wazi na miujiza iliyodhihiri, walikuwa wakisema, «Je binadamu kama sisi wanatuongoza? Hapo wakamkufuru Allah Mtukufu, wakaukanusha ujumbe wa Mitume Wake na wakaipa mgongo haki wasiikubali. Na Allah Mtukufu Hana haja na kuamini kwao wala kuabudu kwao. Na Allah Mtukufu ni Tajiri, Ana utajiri uliotimia usio na mpaka, ni Mwenye kusifiwa kwa maneno Yake, matendo Yake, na sifa Zake, Hawajali wao wala haumdhuru Yeye upotevu wao chochote».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net