Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 5

At-Taghaabun 64:5

التغابن

أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَؤُا۟ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَبْلُ فَذَاقُوا۟ وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Kwani haikukujieni habari ya wale waliokufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani haikukujieni khabari ya walio kufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu. [5]

[5] Zimekwisha wafikieni khabari za walio kufuru kabla yenu, na wao wakameza ubaya wa matokeo wa mambo yao katika dunia. Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je haikuwajia, (enyi washirikina), habari ya wale waliokufuru miongoni mwa watu waliopita kabla yenu, ulipowafikia mwisho mbaya wa ukafiri wao na uovu wa vitendo vyao hapa ulimwenguni, na kuwa kesho Akhera watakuwa na adhabu kali iumizayo?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net