Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 4

At-Taghaabun 64:4

التغابن

يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Maana

Anajua vilivyo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadharani. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anajua viliomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliomo vifuani. [4]

[4] Yeye Mwenyezi Mungu anajua yote yaliomo katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha, na mnayo yaeneza, ikiwa maneno au vitendo. Na Mwenyezi Mungu ametimia ujuzi wake kwa mnayo dhamiria katika nyoyo zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Anajua, kutakasika na kutukuka ni Kwake, kila kilichoko mbinguni na ardhini, na Anakijua mnachokificha, (enyi watu), na mnachokidhihirisha. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa yale yanayodhamiriwa na vifua na kufichwa na nafsi

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net