Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 3

At-Taghaabun 64:3

التغابن

خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ ۖ وَإِلَيْهِ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake. [3]

[3] Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa hikima isiyo na ukomo, na akakuumbeni kwa sura, na akazifanya nzuri sura zenu, kwa kuwa amewafanya wanaadamu ndio viumbe walio nyooka vizuri. Na kwake Yeye ndiyo marejeo Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ameumba mbingu na ardhi kwa hekima kubwa, na Akawaumba nyinyi katika sura nzuri, na Kwake ndio marejeo Siku ya Kiyama, Amlipe kila mtu kwa matendo yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net