Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 10

At-Taghaabun 64:10

التغابن

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marejeo mabaya mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio kufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marudio mabaya. [10]

[10] Na walio ikataa Imani, na wakaikanusha miujiza yetu tuliyo wapa Mitume wetu kuwaunga mkono, hao ndio watu wa Motoni. Watadumu humo. Na marudio maovu ni hayo walio yarudia hao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao wanapinga kwamba Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki na wakazikanusha dalili za kuwa Yeye Ndiye Mola na hoja za uungu Wake Alizowatuma nazo Mitume Wake, hao ni watu wa Motoni, ni wenye kukaa humo milele. Moto huo wa Jahanamu ni marejeo maovu mno watakayofikia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net