Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 11

At-Taghaabun 64:11

التغابن

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۗ وَمَن يُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. [11]

[11] Mja hasibiwi na balaa ila kwa kudra ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumsadiki Mwenyezi Mungu basi humwongoa moyo wake kwendea katika yanayo mpendeza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Halimpati yoyote jambo lolote la shida isipokuwa kwa ruhusa ya Allah Mtukufu na mapitisho Yake na makadirio Yake. Na yoyote anayemuamini Allah Mtukufu, Atauongoza moyo Wake ufuate amri Zake na uridhike na mapitisho Yake. Atauongoza kwenye njia nzuri ya maneno, vitendo na hali. Kwani asili ya uongofu ni moyo, na viungo vinafuata. Na Allah Mtukufu kwa kila kitu ni Mjuzi, hakifichiki Kwake chochote miongoni mwa hivyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net