At-Taghaabun 64:12
التغابنوَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ
Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu. [12]
[12] Na mt'iini Mwenyezi Mungu kwa aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa Ujumbe aliyo kufikishieni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Mkiupuuza ut'iifu huu, basi Yeye hadhuriki kitu kwa mapuuza yenu. Na hakika Mtume wetu hana jukumu juu yake ila kufikisha Utume wake tu kwa uwazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mtiini Allah Mtukufu, (enyi watu), katika yale Aliyoyaamrisha na Aliyoyakataza, na mfuateni Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), katika yale aliyowafikishia kutoka kwa Mola wake. Na iwapo mtaupa mgongo utiifu wenu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake, basi Mjumbe wetu hana madhara yoyote kutokana na kupa mgongo kwenu. Jukumu lake yeye ni kuwafikishia nyinyi yale aliyotumwa kwayo ufikishaji wenye maelezo ya wazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net