Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 18

At-Taghaabun 64:18

التغابن

عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Maana

Mwenye kujua siri na dhahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kujua siri na dhaahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [18]

[18] Yeye ni Mjuzi wa vilivyo fichikana na vinavyo onekana, Mwenye nguvu, Mtenda nguvu, Mwenye hikima katika mipango ya viumbe vyake, Mwenye kuweka kila kitu kwa pahala pake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, ni Mjuzi wa kila lililofichika lisiloonekana na lile lililojitokeza linaloonekana, ni Mshindi Asiye na mshindani, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net