Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 17

At-Taghaabun 64:17

التغابن

إِن تُقْرِضُوا۟ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَـٰعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ

Maana

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni maradufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mstahamilivu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni mardufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukra, Mpole. [17]

[17] Mkitoa katika mambo ya kheri kutoa kwa moyo safi, basi Mwenyezi Mungu atazidisha mardufu thawabu za mlicho toa, na atakusameheni madhambi yenu yaliyo kuponyokeni. Na Mwenyezi Mungu ni Mkuu wa shukrani, na kuwalipa watendao mema, na ni Mpole, hafanyi haraka kuwaadhibu wanao muasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Iwapo mtatoa mali yenu katika njia ya Allah Mtukufu kwa kumtakasia Yeye na kwa moyo mzuri, Atawaongezea Allah Mtukufu thawabu za ambacho mmekitoa na Atawasamehe madhambi yenu. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa kurudisha shukrani kwa watoaji kwa kuwapa malipo mema ya kile walichokitoa, ni Mpole kwa kutoharakisha mateso kwa wanaomuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net