Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 64 · Aya ya 16

At-Taghaabun 64:16

التغابن

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ مَا ٱسْتَطَعْتُمْ وَٱسْمَعُوا۟ وَأَطِيعُوا۟ وَأَنفِقُوا۟ خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Maana

Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na tiini, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio waliofanikiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio walio fanikiwa. [16]

[16] Basi tumieni juhudi zenu na nguvu zenu katika kumcha Mwenyezi Mungu. Na sikieni mawaidha yake, na t'iini amri zake, na toeni katika alicho kuruzukuni kwa ajili ya hicho alicho amrisha kitolewe kwa ajili yake. Na tendeni kheri kwa sababu ya nafsi zenu. Na mwenye kuzuiliwa na Mwenyezi Mungu ubakhili na uchoyo wa roho yake, basi watu kama hao ndio walio jaaliwa kupata kila kheri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Fanyeni juhudi zenu, (enyi Waumini), na tumieni nguvu zenu katika kumcha Allah Mtukufu, na msikilizeni Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), usikilizaji wa kuzingatia na kufikiri, zifuateni amri Zake na myaepuke makatazo Yake na mtoe katika kile Alichowaruzuku Allah Mtukufu, hilo litakuwa bora kwenu. Na atakayeepukana na uchoyo na kubania kilichozidi katika mali, basi hao ndio watakaozipata kheri zote, watakaofaulu kupata kila wanalolitaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Taghaabun

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net