Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 63 · Aya ya 4

Al-Munaafiqoon 63:4

المنافقون

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا۟ تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ ٱلْعَدُوُّ فَٱحْذَرْهُمْ ۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

Maana

Na unapowaona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa. Wao hudhania kila ukelele unaopigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka mbali na haki?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki? [4]

[4] Na ukiwaona miili yao inakupendeza kwa uzuri wao, na wakizungumza unavutika kuwasikiliza kwa utamu wa maneno yao. Kumbe wao juu ya yote hayo nyoyo zao zitupu, hazina Imani ndani yake. Kama magogo yaliyo egemezwa, hayana uhai wowote. Wao hudhania kila linalo zuka basi linawalenga wao, kwa sababu wanaitambua hali yao ya unaafiki. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao. Mwenyezi Mungu kesha wafukuza kwenye rehema yake. Vipi wanavyo iacha Haki wakauendea unaafiki wanao ushikilia?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na unapowatazama wanafiki hawa, yanakufurahisha maumbile yao na mandhari yao, na wanapozungumza unayasikiliza mazungumzo yao kwa ufasaha wa ndimi zao, na hali wao kutokana na utupu wa nyoyo zao kuwa hazina Imani na akili zao kuwa hazina fahamu wala elimu yenye manufaa, ni kama vigogo vilivyotegemezwa kwenye ukuta, visivyokuwa na uhai, wanadhania kila sauti ya ukelele inawashukia wao na ina madhara kwao, kwa kujua kwao uhakika wa hali yao na uoga wao mwingi na hofu iliyojikita nyoyoni mwao. Wao ndio maadui wa kikwelikweli wenye uadui mwingi kwako na kwa Waumini. Basi jihadhari nao, Allah Mtukufu Amewadhalilisha wao na Amewatoa kwenye rehema zake. Basi ni vipi wanaiepuka haki na wanaelekea kwenye yale ambayo wamo ndani yake ya unafiki na upotevu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Munaafiqoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net