Al-Munaafiqoon 63:5
المنافقونوَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوْا۟ رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ
Na wanapoambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni maghfira, huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi. [5]
[5] Na wakiambiwa: Jongeeni, apate Mtume wa Mwenyezi Mungu kukuombeeni msamaha, hutikisa vichwa vyao kwa kejeli, na utawaona wanageuka kwa kiburi hawataki kut'ii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanapoambiwa hawa wanafiki, Njooni huku hali ya kutubia mtake msamaha kwa hayo yaliyotokea kwenu ya maneno maovu na mazungumzo ya ufedhuli, ili Mtume awaombee kwa Allah Mtukufu msamaha wa dhambi zenu, huvigeuza vichwa vyao na wakavitikisa kwa njia ya shere na kiburi. Na utawaona, (ewe Mtume), wanakupa mgongo na huku wanalifanyia kiburi jambo la kufuata yale ambayo walitakiwa wayafuate.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net