Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 63 · Aya ya 3

Al-Munaafiqoon 63:3

المنافقون

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ ثُمَّ كَفَرُوا۟ فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ

Maana

Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo zikazibwa nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote. [3]

[3] Hayo waliyo yafanya ndiyo mazoea ya kudhihirisha yasiyo ya kweli, na kuapa yamini za uwongo, kwa sababu hao wameamini kwa ndimi zao, kisha wakakufuru katika nyoyo zao, basi nyoyo zao zimepigwa muhuri kwa ukafiri huu. Hao hawafahamu yepi ya kuwaokoa na adhabu za Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hilo ni kwa kuwa wao wameamini kijuujuu kisha kindanindani wamekufuru. Ndipo Allah Mtukufu Akapiga mhuri juu ya nyoyo zao kwa ukafiri wao, hivyo basi hawayaelewi yale yenye maslahi kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Munaafiqoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net