Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 63 · Aya ya 2

Al-Munaafiqoon 63:2

المنافقون

ٱتَّخَذُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِنَّهُمْ سَآءَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Wamevifanya viapo vyao ni ngao, na wao wakaizuia Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya. [2]

[2] Wamezifanya yamini zao za uwongo ni kinga, au ngao za kujikingia ili wasichukuliwe kuwa ni makafiri. Basi wakajizuia wenyewe wasiishike Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka. Hakika ni mabaya mno hayo wanayo yatenda ya unaafiki na kujitia imani ya uwongo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ukweli ni kwamba wanafiki wamevifanya viapo vyao wanavyoviapa ni kinga na ngao ya kuwakinga wasihukumiwe na kuadhibiwa, na wamejizuia wenyewe na kuwazuia watu na njia ya Allah Mtukufu iliyonyooka. Kwa kweli wao, ni maovu mno yale waliokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Munaafiqoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net