Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 63 · Aya ya 1

Al-Munaafiqoon 63:1

المنافقون

إِذَا جَآءَكَ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ قَالُوا۟ نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُۥ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ لَكَـٰذِبُونَ

Maana

Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wake, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo. [1]

[1] Ewe Muhammad! Wanapo kujia wanaafiki, wanasema kwa ndimi zao: Tunashuhudia kuwa hakika wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kwamba wewe ni Mtume wake; na Mwenyezi Mungu anashuhudia kwamba wanaafiki hapana shaka ni waongo katika kujidai kwao wanaamini, kwani hawasadiki katika nyoyo zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanapohudhuria wanafiki kwenye kikao chako, (ewe Mtume), husema kwa ndimi zao, Tunakubali kuwa wewe ni Mtume wa Allah Mtukufu, na Allah Mtukufu Anajua kuwa wewe ni mtume wake, na Allah Mtukufu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika ushahidi wao kwako walioudhihirisha na wakauapia kwa ndimi zao na huku wameuficha ukanushaji wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Munaafiqoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net