Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 62 · Aya ya 11

Al-Jumu'a 62:11

الجمعة

وَإِذَا رَأَوْا۟ تِجَـٰرَةً أَوْ لَهْوًا ٱنفَضُّوٓا۟ إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ مِّنَ ٱللَّهْوِ وَمِنَ ٱلتِّجَـٰرَةِ ۚ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Maana

Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki. [11]

[11] Na wakiona bidhaa za biashara, au pumbao lolote hutawanyika kuendea hayo, na wakakuacha wewe umesimama unakhutubu! Waambie: Fadhila na thawabu zilioko kwa Mwenyezi Mungu zina nafuu zaidi kwenu kuliko pumbao na kuliko biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanao toa riziki. Basi itafuteni riziki yake kwa kumt'ii Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi wanapoona baadhi ya Waislamu biashara au chochote miongoni mwa viliwazo vya duniani na pambo lake, hutawanyika kwenda huko na wakakuacha wewe umesimama juu ya mimbari unatoa hutuba. Waambie, (ewe Nabii), Yaliyoko kwa Allah Mtukufu ya thawabu na neema yana manufaa zaidi kwenu kuliko mambo ya lahwu na biashara. Na Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Bora wa wanaoruzuku na kutoa, basi muombeni na mjisaidie kwa kumtii, ili myapate yaliyoko Kwake ya kheri mbili: ya duniani na ya Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jumu'a

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net