Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 62 · Aya ya 10

Al-Jumu'a 62:10

الجمعة

فَإِذَا قُضِيَتِ ٱلصَّلَوٰةُ فَٱنتَشِرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَٱبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Maana

Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na itakapo kwisha Swala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa. [10]

[10] Mkisha maliza kuswali basi tawanyikeni katika nchi kwa ajili ya maslaha yenu, na mtake fadhila za Mwenyezi Mungu. Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenu na ndimi zenu kwa wingi, ili asaa mkafuzu katika kheri za duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi mkisha kuisikia hutuba na mkaitekeleza Swala, tawanyikeni kwenye ardhi na mtafute riziki za Allah Mtukufu, na mtajeni Allah Mtukufu kwa wingi katika hali zenu zote, ili mfaulu kuzipata kheri mbili: za (duniani na za Akhera).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jumu'a

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net