Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 60 · Aya ya 13

Al-Mumtahana 60:13

الممتحنة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَوَلَّوْا۟ قَوْمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا۟ مِنَ ٱلْـَٔاخِرَةِ كَمَا يَئِسَ ٱلْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْقُبُورِ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wa kusaidiana nao katika watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama wamekwishakata makafiri miongoni mwa watu wa makaburini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyo wakatia tamaa watu wa makaburini. [13]

[13] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake, msiwafanye kuwa rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewaghadhibikia. Hao wamekata tamaa na Akhera na yote yatakao kuwapo huko, ya kulipwa na kuhisabiwa, kama makafiri walivyo kata tamaa kufufuliwa waliomo makaburini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake! Msiwafanye wale ambao Allah Mtukufu Amewakasirikia kwa ukafiri wao kuwa ni marafiki na vipenzi, kwani hao washakata tamaa kupata thawabu za Allah Mtukufu kesho Akhera, kama makafiri walio makaburini walivyokata tamaa ya kupata rehema za Allah Mtukufu huko Akhera, watakaposhuhudia ukweli wa mambo na wakajua ujuzi wa yakini kuwa hawatakuwa na fungu lolote huko, au kama walivyokata tamaa makafiri kufufuliwa wafu wao- walio makaburini- kwa kuitakidi kwao kuwa hakuna kufufuliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mumtahana

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net