As-Saff 61:1
الصفسَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۖ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [1]
[1] Kila kiliomo katika mbingu na kiliomo katika ardhi kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa ni laiki yake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kuvishinda vitu vyote, Mwenye hikima iliyo fika ukomo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Vimemtakasa Allah Mtukufu na kila kisichonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na Yeye ni Mshindi Ambaye hakuna mwenye kushindana naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net