Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 60 · Aya ya 12

Al-Mumtahana 60:12

الممتحنة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلْمُؤْمِنَـٰتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِٱللَّهِ شَيْـًٔا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَـٰدَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَـٰنٍ يَفْتَرِينَهُۥ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِى مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَٱسْتَغْفِرْ لَهُنَّ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanao uzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira, Mwenye kurehemu. [12]

[12] Ewe Nabii! Wakikujia wanawake Waumini kukuahidi kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatwauwa watoto wao, wala hawatawabandikiza waume zao watoto wao (wa haramu) kwa uzushi na uwongo wanao uzua baina ya mikono yao na miguu yao. (yaani matumboni mwao, au kwa ndimi zao na tupu zao); wala hawendi kinyume nawe katika jambo jema unalo waitia, basi pokea ahadi zao juu ya hayo, na waombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na kurehemu. (Mtume s.a.w. haamrishi ila jema, lakini sharia hapo inasema kuwa mtawala yeyote hut'iiwa akiamrisha jema tu. Ama kwa lilio ovu, Mtume s.a.w. amesema: "Hapana kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba.")

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Wakiwajia wanawake wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na kuwaahidi kuwa hawatamshirikisha Allah Mtukufu katika kumuabudu, wala hawataiba chochote, wala hawatazini, wala hawataua watoto wao baada ya kuzaliwa au kabla yake, wala hawatawanasibishia waume zao watoto wasiotokana na wao, wala hawataenda kinyume na wewe katika jema unalowaamrisha kwalo, basi waahidi kwa hayo na uwaombee msamaha kutoka kwa Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kusamehe dhambi za waja Wake wenye kutubia, na ni Mwenye kuwarehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mumtahana

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net