Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 4

Al-An'aam 6:4

الأنعام

وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ مِّنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ

Maana

Na haiwajii ishara miongoni mwa ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa walikuwa wakiipa mgongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na haiwafikii hata ishara moja katika ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa wenye kuipa nyongo. [4]

[4] Wala washirikina hawaletewi ishara yoyote katika ishara za Muumbaji wao zinazo shuhudia Umoja wake na ukweli wa Mitume wake, ila wao huikataa na kuibeza ishara hiyo, wala hawaizingatii, wala hawaitii maanani!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Makafiri hawa Ambao wanamshirikisha mwingine na Allah Mtukufu, (Aliyetukuka,) wamejiwa na hoja zilizo wazi na dalili dhahiri juu upweke wa Allah Mtukufu, (Aiyetukuka) na kuwa juu, na ukweli wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) juu ya utume wake na yale aliyokuja nayo. Lakini punde tu yalipowajia waliyaepuka na kukataa kuyakubali na wasiyaamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net