Al-An'aam 6:3
الأنعاموَهُوَ ٱللَّهُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَفِى ٱلْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ
Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi. Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini. Anajua ya ndani yenu na ya nje yenu. Na anajua mnayo yachuma. [3]
[3] Na ni Yeye peke yake anaye stahiki kuabudiwa katika mbingu na katika ardhi. Anajua kila mnacho kificha na mnacho kionyesha. Na anajua yote mnayo yatenda, Naye atakulipeni kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki mbinguni na ardhini. Na miongoni mwa dalili za uungu wake ni kwamba Yeye Anayajua yote mnayoyaficha, enyi watu, na mnayoyadhihirisha na Anayajua matendo yenu yote, mazuri na mabaya. Na kwa ajili hii, Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye Mola Anayestahiki kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net