Al-An'aam 6:2
الأنعامهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰٓ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُۥ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ
Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo, kisha akawahukumia muda, na muda maalumu uko kwake tu. Kisha nyinyi mnatia shaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni ajali, na muda maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka. [2]
[2] Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuanzeni kwa kukuumbeni kutokana na udongo. Kisha akamkadiria kila mmoja wenu ana zama maalumu za uhai, kisha uhai huo unakwisha kwa kufa. Na muda maalumu ulio wekwa wa kufufuliwa kutoka kaburini uko kwake Yeye pekee. Kisha tena enyi makafiri! Mnabisha uwezo wa Mwenyezi Mungu kufufua, na kustahiki kwake peke yake kuabudiwa?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye Ambaye Alimuumba baba yenu Ãdam kutokana na udongo na nyinyi mnatokana na kizazi chake, kisha Akaandika muda wa kuishi kwenu katika uhai huu wa kilimwengu, na Akaandika muda mwingine maalumu hakuna aujuwao isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, nayo ni Siku ya Kiyama. Kisha nyinyi baada ya haya mnashuku juu ya uwezo wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, wa kufufua baada ya kufa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net