Al-An'aam 6:5
الأنعامفَقَدْ كَذَّبُوا۟ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنۢبَـٰٓؤُا۟ مَا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Basi hakika walikwishaikadhibisha haki ilipowajia. Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wameikanusha Haki ilipo wajia. Basi zitawajia khabari za yale waliyo kuwa wakiyakejeli. [5]
[5] Wao wameikanusha Qur'ani ilipo wajia, na ilhali hiyo ni Haki isiyo changanyika na upotovu! Basi yatawapata mateso ya duniani, na adhabu ya Akhera, kama ilivyo eleza Qur'ani. Na hapo utawabainikia ukweli wa onyo lake walilo kuwa wakilifanyia maskhara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Makafiri hawa waliikataa haki ambayo alikuja nayo Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) na wakawafanyia shere walinganizi wake kwa sababu ya ujinga walionao kuhusu Allah Mtukufu na kughurika kwao na muhula Aliowapa. Basi watakuja kuyaona yale waliyoyafanyia shere kuwa ni haki na ni kweli. Na Allah Mtukufu Atawabainishia wakanushaji urongo wao na uzushi wao na awalipe kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net