Al-An'aam 6:18
الأنعاموَهُوَ ٱلْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ
Naye ndiye Mwenye nguvu za ushindi juu ya waja wake, naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, na ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari zote. [18]
[18] Yeye ndiye Mwenye kushinda kwa uwezo wake, Aliye juu, juu ya waja wake, Aliye sifika kwa hikima katika kila alifanyalo, Mwenye kuvizunguka kwa ujuzi wake vinavyo onekana na vinavyo fichikana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mwenye kutendesha nguvu, Aliye juu ya waja Wake. Shingo zimemdhalilikia na majabari wamenyongeka Kwake. Yeye Ndiye Mwenye hekima Anayeweka vitu mahali pake kulingana na hekima Yake. Ndiye Mtambuzi Ambaye hakuna kitu chenye kufichika Kwake. Na mwenye kusifika na sifa hizi inapasa asishirikishwe. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya ujuu kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kuwa Yuko juu ya ya viumbe vyake vyote; ujuu wa aina zote unaonasibiana na utukufu Wake, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net