Al-An'aam 6:17
الأنعاموَإِن يَمْسَسْكَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Na ikiwa Mwenyezi Mungu atakugusa kwa madhara, basi hapana wa kuyaondoa isipokuwa Yeye. Na ikiwa atakugusa kwa heri, basi Yeye ndiye Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea hayo ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri, basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu. [17]
[17] Mwenyezi Mungu akikupatiliza kwa ovu, basi hapana wa kuliondoa hilo ila Yeye Mwenyewe. Na akikupa kheri basi hapana awezae kuirudisha fadhila yake, kwani Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Akikupatia Allah Mtukufu jambo la kukudhuru, kama ufukara na ugonjwa, hakuna mwenye kuliondoa hilo isipokuwa Yeye; na Akikupatia zuri, kama utajiri na afya, hakuna mwenye kuondoa wema wake na hakuna mwenye kuzuia mapitisho Yake, kwani Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, ni muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net