Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 144

Al-An'aam 6:144

الأنعام

وَمِنَ ٱلْإِبِلِ ٱثْنَيْنِ وَمِنَ ٱلْبَقَرِ ٱثْنَيْنِ ۗ قُلْ ءَآلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلْأُنثَيَيْنِ أَمَّا ٱشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ ٱلْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَآءَ إِذْ وَصَّىٰكُمُ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ ٱلنَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na katika ngamia ni wawili, na katika ng'ombe ni wawili. Sema: Je, ameharamisha haya madume yote mawili au majike wawili haya, au walio matumboni mwa majike haya? Au, nyinyi mlishuhudia Mwenyezi Mungu alipowausia haya? Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu uoongo, ili awapoteze watu bila ya elimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

.Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu. [144]

[144] Na Mwenyezi Mungu ameumba ngamia namna mbili, dume na jike, na ng'ombe namna mbili mbili vile vile. Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanya: Nini sababu ya kuwaharimisha hao mlio harimisha kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa wao ni madume? Sivyo hivyo; kwa sababu pengine mnahalalisha madume! Au ni kwa kuwa majike? Pia sio hivyo, kwa sababu mnahalalisha majike wakati mwingine! Au kwa kuwa wana watoto matumboni mwao? Pia sio hivyo, kwa sababu hamkuharimisha watoto walio matumboni daima. Nanyi mnadai kuwa kuharimisha huku kunatokana na Mwenyezi Mungu! Nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuharimisheni haya na mkamsikia makatazo yake? Kabisa hayo hayakuwa. Wacheni mlio nayo; kwani hiyo ni dhulma. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko mwenye kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamnasibisha nayo mambo yasiyo toka kwake, wala hayana tegemeo lolote la ki-ilimu la kutegemea, bali huyo anataka kuwapotosha watu tu! Mwenyezi Mungu hawawafikishi wenye kudhulumu wakikhiari njia ya upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na aina nne nyingine ni aina mbili za ngamia, waume na wake, na aina mbili za ng’ombe, waume na wake. Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hao, «Kwani Allah Mtukufu Amewaharamisha madume wawili au majike wawili? Au Ameharamisha vilivyomo ndani ya matumbo ya majike wawili, wawe madume au majike? Au mlikuwa, enyi washirikina, mupo pindi Allah Mtukufu Alipowapa wasia wa uharamu huu wa wanyama Howa? Hakuna dhalimu mbaya zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo, ili awapotoshe watu, kwa ujinga wake, na njia ya uongofu. Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Hamuelekezi kwenye muelekeo wa sawa yule aliyekiuka mpaka wake, akamzulia urongo Mola wake na akawapoteza watu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net