Al-An'aam 6:143
الأنعامثَمَـٰنِيَةَ أَزْوَٰجٍ ۖ مِّنَ ٱلضَّأْنِ ٱثْنَيْنِ وَمِنَ ٱلْمَعْزِ ٱثْنَيْنِ ۗ قُلْ ءَآلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلْأُنثَيَيْنِ أَمَّا ٱشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ ٱلْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّـُٔونِى بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
(Amewaumbia) majozi manane: katika kondoo ni wawili, na katika mbuzi ni wawili. Sema: Je, ameharamisha madume wawili hawa au majike wawili hawa, au wale walio matumboni mwa majike yote mawili haya? Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli. [143]
[143] Mwenyezi Mungu ameumba katika kila namna ya nyama hoa dume na jike. Hizo basi ni namna nane. Kondoo namna mbili, mbuzi namna mbili. (ngamia na ng'ombe wametajwa katika Aya inayo fuata.) Ewe Muhammad! Waambie washirikina kukanya hayo waliyo yaharimisha: Nini sababu ya kuharimisha katika hawa kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa madume? Au kwa kuwa ni kuwa matumboni ya mama zao? Hayo hayawezi kuwa hivyo, kwa sababu nyinyi hamkuharimisha watoto waliomo tumboni kabisa!! Nambieni kwa mategemeo baraabara, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika kuhalalisha na kuharimisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanyama hawa ambao Allah Mtukufu Amewaruzuku waja Wake, miongoni mwa ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, ni aina nane: nne kati ya hizo ni mbuzi na kondoo, nao ni kondoo: waume na wake, na mbuzi: waume na wake. Sema, ewe Mtume, uwaambie hao washirikina, «Kwani Allah Mtukufu Amewaharamisha madume wawili wa mbuzi na kondoo?» Wakisema, «Ndio», watakuwa wamesema urongo kuhusu hilo. Sababu wao hawalifanyi kila dume la kondoo na mbuzi kuwa ni haramu. Na waambie, «Kwani Allah Mtukufu Amewaharamisha majike wawili wa mbuzi na kondoo?» wakisema, «Ndio», watakuwa pia wamesema urongo. Sababu wao hawamuharamishi kila mwanambuzi na mwanakondoo mke. Na sema uwaambie, «Kwani Allah Mtukufu Amewaharamisha watoto walio matumboni mwa majike wawili wa mbuzi na kondoo walio na mimba?» Wakisema, «Ndio.» Watakuwa wamesema urongo pia. Kwani hawaiharamishi kila mimba ya namna hiyo. niambieni kwa misingi ya elimu inayoonesha usahihi wa msimamo wenu, mkiwa ni wakweli katika hayo mnayoyanasibisha kwa Mola wenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net