Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 142

Al-An'aam 6:142

الأنعام

وَمِنَ ٱلْأَنْعَـٰمِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

Maana

Na katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na wengine wadogo. Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri. [142]

[142] Na Mwenyezi Mungu ameumba katika nyama hoa, nao ni ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, wale wanao beba mizigo yenu, na wale ambao katika sufi yao na manyoya yao na nyewele zao mnatoa matandiko. Na hiyo ni riziki aliyo kujaalieni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni alicho kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msimfuate Shetani na marafiki zake katika kuzua vya halali na haramu, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa Jahiliya! Hakika Shetani hakutakiini kheri, kwa sababu yeye ni adui yenu, mwenye uadui dhaahiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Ameleta katika wanyama wale ambao wametayarishwa kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wakubwa na ni warefu, kama ngamia. Na miongoni mwao kuna waliotayarishwa si kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wadogo na wafupi, kama ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kuleni wale Aliyowahalalishia nyinyi Allah Mtukufu miongoni mwa hawa wanyama, wala msiwaharamishe wale Aliyowahalalisha miongoni mwao kwa kufuata njia za Shetani kama walivyofanya washirikina. Hakika Shetani, kwenu nyinyi, ni adui mwenye uadui wa wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net