Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 141

Al-An'aam 6:141

الأنعام

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَ جَنَّـٰتٍ مَّعْرُوشَـٰتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَـٰتٍ وَٱلنَّخْلَ وَٱلزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيْتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَـٰبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَـٰبِهٍ ۚ كُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثْمَرَ وَءَاتُوا۟ حَقَّهُۥ يَوْمَ حَصَادِهِۦ ۖ وَلَا تُسْرِفُوٓا۟ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْمُسْرِفِينَ

Maana

Na Yeye ndiye aliyeyaanzisha mabustani yenye kutambaa kwenye fito, na yasiyotambaa kwenye fito, na mitende, na mimea yenye vyakula mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa kupitiliza. Hakika Yeye hawapendi watumiao kwa kupitiliza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo. [141]

[141] Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye umba bustani za matunda. Ipo miti inayo pandwa na kuegemezwa juu ya chanja, na ipo isiyo hitajia chanja. Na ameumba mitende, na mimea mingine inayo toa matunda yanayo khitalifiana kwa rangi, na utamu, na sura, na harufu na mengineyo. Na ameumba mizaituni, na makomamanga (makudhumani), yenye kushabihiana katika baadhi ya sifa zake, na isiyo shabihiana, ijapo kuwa udongo huenda ukawa ule ule, na yote ikawa inanyweshwa na maji yale yale. Basi kuleni matunda yake mkipenda, na toeni sadaka yake yanapo wiva na kuyachuma. Wala msifanye fujo katika kula, mkajidhuru wenyewe, na mkawadhuru mafakiri katika kuwanyima haki yao. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watumiao kwa fujo, katika mwendo wao na vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Aliyewaanzishia mashamba: miongoni mwa mimea yake kuna ile iliyoinuliwa juu ya ardhi na kuegemezewa vitu vyingine, kama mizabibu, na miongoni mwayo kuna isiyoinuliwa, bali inasimama yenyewe kwenye vigogo vyake, kama mitende na miti mingine ya mazao. Mimea yote hiyo ikiwa ina tamu tafauti. Mizabibu na mikomamanga, maumbile yake yanafanana na matunda yake yanatafautiana tamu yake. Kuleni, enyi watu, matunda yake na mtoe Zaka zake zilizolazimishwa kwenu siku mnapoyavuna na kuyatungua, na msiikiuke mipaka ya usawa katika kutoa mali na kula chakula na mengineyo. Hakika Yeye, Allah Mtukufu, Hawapendi wenye kukiuka mipaka Yake kwa kutumia mali katika njia zisizokuwa zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net