Al-An'aam 6:138
الأنعاموَقَالُوا۟ هَـٰذِهِۦٓ أَنْعَـٰمٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَـٰمٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَـٰمٌ لَّا يَذْكُرُونَ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهَا ٱفْتِرَآءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Nao walisema: "Mifugo hawa na mimea ni miiko. Hawavili isipokuwa tumtakaye" - kwa madai yao tu. Na mifugo wengine imeharamishwa migongo. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, kwa kumzulia uongo tu. Atawalipa kwa hayo ya uongo waliyokuwa wakiyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia. [138]
[138] Na katika mawazo yao ni kusema kwao: Ngamia hawa, na ng'ombe hawa, na mbuzi na kondoo hawa, na mazao haya ya mimea, ni marfuku. Hayali mtu ila wamtakaye katika utumishi wa masanamu. Hayo ni kwa madai yao ya uwongo, wala hayatokani na Mwenyezi Mungu. Na pia husema: Ngamia hawa wameharimishwa migongo yao, basi hapana ruhusa mtu kuwapanda. Nao juu ya hao hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wanapo wachinja hao ngamia, na ng'ombe, na mbuzi na kondoo. Na hayo ni kwa kule kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ushirikina wao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa adhabu huko Akhera kwa sababu ya uzushi wao, na kuharimisha kwao vitu ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharimisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema washirikina kwamba ngamia hawa na mazao haya ni vitu haramu; haifai kuvila kwa mtu yoyote isipokuwa yule wanayemruhusu, kulingana na madai yao, miongoni mwa wasimamizi wa mizimu na wengineo. Na hawa ni ngamia ambao ilipewa heshima migongo yao, haifai kupandwa wala kubebeshwa vitu juu yake kwa namna yoyote. Na hawa ni ngamia ambao hawawatajii jina la Allah Mtukufu, Aliyetukuka, katika jambo lolote linalowahusu wao. Waliyafanya hayo kwa urongo utokao kwao, kumzulia Allah Mtukufu. Allah Mtukufu Atawalipa kwa urongo waliokuwa wakimzulia Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net