Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 139

Al-An'aam 6:139

الأنعام

وَقَالُوا۟ مَا فِى بُطُونِ هَـٰذِهِ ٱلْأَنْعَـٰمِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَآءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٌ

Maana

Na walisema: Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni vya wanaume wetu tu, na vimeharamishwa kwa wake zetu. Lakini wakiwa nyamafu, basi wanashirikiana ndani yake. Atawalipa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharimishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Mwenyezi Mungu atawalipa kwa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hikima, Mwenye kujua. [139]

[139] Na katika mawazo yao ya uwongo hawa washirikina ni kuwa wanasema: Viliomo matumboni mwa wanyama walio watenga, walio zuwiwa wasichinjwe wala wasipandwe - viliomo matumboni mwao, yaani watoto, wanafaa kuliwa na wanaume, na haramu kwa wanawake. Na juu ya hivyo akizaliwa naye kesha kufa wote wanashirikiana wanakula! Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa kwa uwongo wao walio mzulia kwa kitendo chao. Kwani wanadai kuwa kuharimishwa huku kunatokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu, na ni Mwenye hikima. Vitendo vyake vyote ni kwa mujibu wa hikima. Naye atawalipa wenye dhambi kwa dhambi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walisema washirikina, «Watoto waliomo ndani ya wanyama howa, wakizaliwa wakiwa hai, ni halali tu kwa wanaume kati yetu na ni haramu kwa wanawake miongoni mwetu.» Na wakizaliwa nao wamekufa wanashirikiana katika kuwatumia. Allah Mtukufu Atawatesa kwa kujiwekea sheria za kuhalalisha na kuharamisha ambazo Allah Mtukufu hakuziruhusu. Hakika Yeye Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo ya viumbe Wake, Mjuzi sana kuhusu wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net