Al-An'aam 6:108
الأنعاموَلَا تَسُبُّوا۟ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّوا۟ ٱللَّهَ عَدْوًۢا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Wala msiwatukane hao ambao wao wanawaomba badala ya Mwenyezi Mungu, nao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao ni kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda. [108]
[108] Enyi Waumini! Msiyatukane masanamu ya washirikina wanayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, isije chuki yao kwa hayo ikawapelekea hasira ya kumtukana Mwenyezi Mungu kwa uadui na ujinga. Kama tulivyo wapambia hawa kupenda masanamu yao, kila umma una a'mali yake kwa mujibu wa makdara yao. Na marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake Siku ya Kiyama. Naye atawaeleza khabari ya vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na msiyatukane, enyi Waislamu, masanamu ambyo washirikina wanayaabudu, ili hilo lisije likawafanya wao wamtukane Allah Mtukufu kwa ujinga na kwa uadui, bila ya kuwa na ujuzi. Na kama tulivyowapambia hawa matendo yao mabaya, yakiwa ni mateso kwao kwa uchaguzi wao mbaya, ndivyo tulivyowapambia kila umma matendo yao. Kisha marejeo yao wote ni kwa Mola wao; hapo Allah Mtukufu Awaambie matendo yao waliokuwa wakiyatenda ulimwenguni kisha Awalipe kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net